William Mpanju- Biharamulo, KAGERA
Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi chini ya Shirika la Compation International Tanzania limemkabidhi nyumba yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 13.5 mtoto Ziyuni Maisha Tumaini mwenye umri wa miaka 10 mkazi wa Kijiji cha Nyakatuntu kata ya Biharamulo mjini mkoani Kagera.
Ziyuni Maisha Tumaini alikuwa akiishi mazingira magumu na mama yake mzazi kutokana na kukosa makazi.

Mratibu wa Kituo cha Maendeleo ya kijana na mtoto cha Kanisa la KKKT chini ya Shirika la Compation International Tanzani Bi. Eles Ezra amesema mtoto anapaswa kulelewa katika malezi na makuzi bora kwa kuzingatia sera na mlezi Bora kwa mtoto.

Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Prof. Josephat Rweyemamu na mchungaji wa Kanisa la KKKT jimbo la Kusini C amewataka wazazi wa mtoto huyo kuilinda na kuitunza na kuishia kwa amani na kamwe nyumba hiyo siyo ya wazazi bali ni ya mtoto na usiwe uwanja wa Vita.

