
Kocha wa timu ya Tanzania (Taifa Stars) Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesema watabuni mbinu bora zaidi na kuzitumia kwenye mechi dhidi ya Madagascar itakayochezwa Jumamosi, Agosti 09, 2025, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Kocha Hemedi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 08, 2025 na kueleza kuwa, kikosi hicho kitatumia mbinu hizo mapema mchezoni ili kuhakikisha wanashinda.
Vilevile amebainisha kuwa, timu ya Tanzania imejipanga vyema kwa mechi zinazofuata na watacheza kila mechi kama fainali ili kuchukua ubingwa wa michuano ya CHAN 2024.
Kwa upande wake golikipa Aishi Manula amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwapa hamasa zaidi katika mchezo huo.