
Ciara ameingiza wimbo wake “Low” aliomshirikisha Diamond Platnumz kwenye orodha ya kazi zinazotafutwa kuzingatiwa kwa Tuzo za Grammy.
Kupitia kampeni yake rasmi ya For Your GRAMMY® Consideration, Ciara amewasilisha “Low” kama mgombea kwenye vipengele vya ‘Best Music Video’ na ‘Best African Music Performance’.
Mbali na “Low”, albamu yake CiCi imependekezwa kwa Best Progressive R&B Album, huku wimbo “Ecstasy” aliomshirikisha Normani na Teyana Taylor ukitazamwa katika vipengele vya Best R&B Song na Best R&B Performance.
Endapo “Low” itafanikiwa kupata uteuzi rasmi, itakuwa ni hatua kubwa kwa Diamond Platnumz msanii wa kwanza wa Afrika Mashariki kushirikishwa katika kampeni ya Grammy ya kiwango hicho kupitia ushirikiano na staa wa kimataifa.