ASAP Rocky amefunguka hivi karibuni kuhusu jinsi mama yake, Renee Black, alivyokuwa na imani kuwa angefaa kuwa na staa wa kimataifa, Rihanna, miaka mingi kabla ya uhusiano wao kuanza.
Rocky amesema mama yake mara nyingi alimwambia, “Nataka uwe na Riri”, hata wakati yeye alidhani walikuwa marafiki tu. Mwanzo alidhani ni utani, lakini sasa anakiri kuwa mama yake alikuwa na hisia sahihi.
Mapenzi yao yalianza rasmi mwaka 2020, na tangu hapo wamejenga familia pamoja na kuwa moja wapenzi wanaofuatiliwa zaidi kwenye dunia ya muziki.