
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa limejiandaa kikamilifu za kiusalama kuelekea mchezo mkubwa wa soka kati ya timu ya Simba na Yanga utakaochezwa Kesho uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo SACP Jumanne Muliro amesema vyombo vya dola kwa kushirikiana na wananchi, vinaendelea kuhakikisha hali ya usalama jijini humo inabaki kuwa shwari
Kamanda Muliro amesema kutokana na mchezo huo kukutanisha mashabiki kutoka ndani na je ya Dares Salaam hairuhusiwi mtu yeyote kufika uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa askari maalum waliopangwa kwa ajili ya kulinda amani
Jeshi la Polisi limetoa wito kwa mashabiki wa soka kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani kabla, wakati na baada ya mchezo huo na kwamba hatua kali za kiesheria zitachukuliwa dhidi ya watakao vunja sheria