
Wasifu wa Papa mchungaji, mwalimu wa ubinadamu, mwenye uwezo wa kumwilisha uso wa Kanisa la Kisamaria, karibu na mahitaji na majeraha ya wanadamu, waelezwa katika Kusanyiko la kumi na mbili na la mwisho la Makadinali lililofanyika jana tarehe 6 Mei 2025 kupisha Kongamano la makdinali la kumteua papa ambalo limeanza leo tarehe 7 Mei 2025.
Kongamano hili lilihudhuriwa na makadinali 173, kati yao 130 wakiwa ni wapiga kura. Kulikuwa na mapendekezo 26, yakihusisha mada nyingi.
Miongoni mwa mada kuu zilizojitokeza ni uthibitisho kwamba mengi ya mageuzi yaliyopendekezwa na Baba Mtakatifu Francisko yanahitaji kuendelezwa: mapambano dhidi ya unyanyasaji, uwazi wa kiuchumi, upangaji upya wa “Curia”, sinodi, kujitolea kwa amani na kujali uumbaji. Wajibu wa Kanisa katika maeneo haya unasikika kwa kina na kushirikiwa.
Mada kuu ya tafakari hiyo ilikuwa ya Ushirika, iliyoonyeshwa kama wito muhimu kwa Papa mpya. Wasifu wa Papa mchungaji, mwalimu wa ubinadamu, mwenye uwezo wa kumwilisha uso wa Kanisa la Kisamaria, karibu na mahitaji na majeraha ya wanadamu, ulielezwa. Katika nyakati zenye vita, ghasia na mgawanyiko mkubwa, hitaji kubwa linaonekana kwa kiongozi wa kiroho ambaye hutoa rehema, sinodi na matumaini.
Baadhi ya michango pia ilishughulikia maswali ya asili ya kisheria, kutafakari juu ya uwezo wa Papa.
Mada ya migawanyiko ndani ya Kanisa na katika jamii, na jinsi Makadinali wanavyoitwa kutekeleza wajibu wao kuhusiana na Upapa, ilishughulikiwa.
Siku ya Maskini Duniani nayo ilitajwa, itakayofanyika Jumapili kabla ya maadhimisho ya Kristo Mfalme; ilisisitizwa kwamba matukio haya mawili yanaweza kufasiriwa kwa uhusiano wa moja kwa moja, kwa kutambua uwepo hai wa Kristo katika maskini na kukumbuka kwamba ufalme wa kweli wa Injili unadhihirika katika huduma.
Makadinali walizungumza juu ya hitaji la kufanya mikutano ya umoja wa Makadinali kuwa muhimu zaidi wakati wa Consistories (Baraza la Makadinali) na kukuza uanzishwaji wa Kikristo na malezi endelevu kama vitendo halisi vya kimisionari.
Wafia-imani wa imani walikumbukwa, hasa katika nchi zile ambako Wakristo huteswa au kunyimwa uhuru wa kidini. Miongoni mwa dharura za kichungaji, dhamira ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, inayotambuliwa kama changamoto ya kimataifa na ya kikanisa, ilisisitizwa pia.
Makadinali walitafakari tena tarehe ya kuadhimisha Pasaka, Baraza la Nikea na majadiliano ya kiekumene.
Kutaniko lilimalizia kwa kusomwa kwa tangazo rasmi: rufaa iliyoelekezwa kwa wahusika waliohusika katika migogoro mbalimbali ya kimataifa. Makadinali waliomba usitishaji vita wa kudumu na kuanza kwa mazungumzo ya kuleta amani ya haki na ya kudumu, kwa kuheshimu utu wa binadamu na manufaa ya wote.
Wakati wa mkutano huo wa asubuhi, kubatilishwa kwa Pete ya Wavuvi na muhuri wa kuongoza kulifanyika.
Hatimaye leo makadinali wamekwishakusanyika tayari kwa kuanza mchakato wa kumpata papa mpya.
Imetafsiriwa na Redio Kwizera, Jukwaa la Matumaini.