Serikali imetangaza kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Bima ya Afya kwa Wote (BAW), hatua inayolenga kuwaondolea mzigo wa gharama za matibabu wananchi wasio na uwezo wakiwemo wazee, watoto, wajawazito na watu wenye ulemavu, ambao gharama zao zitabebwa na Serikali.
Waziri amesema Kitita cha Huduma Muhimu kwa awamu ya kwanza kitaanza kutumika Januari 26, 2026, kwa kundi la wananchi watakaogharamiwa na Serikali.
Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa amezungumza hayo leo Januari 23, 2026 wakati wa kikao kazi cha kitaifa cha kujadili utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.
Waziri amesema awamu ya kwanza ya utekelezaji itaambatana na kuanza kutumika kwa Kitita cha Huduma Muhimu, kitakachotolewa na Skimu za Bima ya Afya wakilenga makundi yaliyo hatarini ili kupata huduma za afya bila kikwazo cha fedha.
Aidha amesemBei ya kitita hicho ni Sh150,000 kwa kaya isiyozidi watu sita, kikiwa kinazingatia utaratibu wa rufaa katika vituo vya afya vilivyoingia mkataba na Skimu za Bima ya Afya.