
Mitandao ya kijamii imechafuka baada ya rapa Nicki Minaj kutoa kauli nzito inayomshambulia Keyshia Ka’Oir, mke wa rapa Gucci Mane.
Kupitia ukurasa wake wa X, Nicki aliandika ujumbe uliozua taharuki kubwa, akisema:
Mke wa Gucci amekuwa akijaribu kuwa kama yeye kwa miaka mingi. Amekuwa akitamani umaarufu kwa muda mrefu. Yupo pale kumweka Gucci katika utulivu. Gucci hamtaki Debra Antney, hawataki awe karibu nami, lakini sasa yupo. Charlamagne ni tapeli anayetumia iHeartRadio kwa njama chafu dhidi ya familia zisizo na hatia.
Kauli hiyo imeibua hisia kali, hasa kwa kuwa Nicki ametaja majina makubwa kama Debra Antney, aliyewahi kuwa meneja wake na Gucci Mane, pamoja na mtangazaji Charlamagne Tha God, akimtuhumu kutumia vyombo vya habari kudhoofisha wasanii.
Mashabiki wamehusisha ujumbe huu na mvutano wa muda mrefu kati ya Nicki na Keyshia Ka’Oir, ambao unatokana na kufanana kwao katika aina ya uvaaji na historia ya kibiashara na Gucci Mane. Wengine wanasema huu ni mwendelezo wa bifu lililofichwa kwa muda mrefu kwenye kiwanda cha hip-hop.
Hadi sasa, Keyshia Ka’Oir hajajibu moja kwa moja, lakini kwenye mahojiano yake mapya na The Breakfast Club, alisema anamuepusha Gucci na mitandao ya kijamii akiona mambo hayapo sawa, akisisitiza kuwa afya ya akili ya mumewe ndiyo kipaumbele chake.