
Keyshia Ka’Oir, mke wa rapa #GucciMane, amepokea sifa nyingi kwa jukumu muhimu analolichukua katika kumlinda mumewe kutokana na changamoto za afya ya akili.
Kwenye mahojiano, Keyshia ameeleza kuwa anamtenga Gucci Mane na mitandao ya kijamii pale anapogundua mambo hayako sawa.
Anabadili password, kuondoa apps, na kuhakikisha kuwa mumewe haathiriki kwenye majadiliano yanayoweza kuathiri hali yake ya akili. Hii ni njia yake ya kuhakikisha jamii haioni mabadiliko ya mumewe.
Keyshia amesema kuwa anafahamu dalili za vipindi vigumu vya Gucci Mane kama vile kutokula, kutokulala, au kuacha kuongea, na anachukua hatua mara moja kumsaidia. Hatua hizi ni mfano wa utajiri wa kweli, sio mali pekee, bali utulivu wa akili na heshima ambayo mwanaume anapewa kama kichwa cha familia.