
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Dkt. Abel Nyamahanga amesema hakuna Mkuu wa Shule au Mwalimu Mkuu mwenye mamlaka ya kumzia mwanafunzi kushiriki kwenye michezo mbalimbali ndani ya Wilaya hiyo.
Dkt. Nyamahanga amesema hayo wakati akifungua mashindano ya michezo ya UMISETA na UMITASHUMITA ngazi ya Wilaya kwenye Shule za Msingi na Sekodari iliyozinduliwa leo hii katika chuo Cha ualimu Katoke.
Amesema kuwa Serikali itaendeleza jitihada za michezo kwenye shule za Msingi na Sekodari ikiwemo kuibua vipaji vya wanafunzi pamoja na kujenga Viwanja vya michezo.
Awali Afisa Utamaduni na Michezo Wilaya ya Muleba Bw. Denis Joseph amesema jumla ya wanafunzi 240 wameshiriki michezo hiyo kutoka Kanda sita ambazo ni Kimwani, Kamachumu, Izigo Muleba, Nshamba na Kanda ya Visiwani huku katika mashindano ya UMITASHUMITA ngazi ya Wilaya Kanda ya Kimwani imeibuka mshindi wa jumla na kukabidhiwa kombe la ushindi.