
Mwanamuziki maarufu wa R&B, D’ Angelo, ambaye jina lake halisi ni (Michael Eugene Archer) amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 51.
Mwanamziki huyo amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa Saratani ya kongosho.
D’Angelo anayefahamika kwa vibao kama “Brown Sugar” na Untitled (How Does It Feel) alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa muziki wa Neo-soul, akichanganya mitindo ya Gospel, funk na R&B kwa umahiri mkubwa uliomtofautisha na wasanii wengine.
Kupitia album zake maarufu kama Brown sugar (1995), Voodoo (2000)- iliyompa tuzo ya Grammy na Black Messiah (2014) D’Angelo alibadilisha kabisa sura ya muziki wa kisasa na urithi mkubwa katika tasnia ya muziki duniani.
Katika safari yake ya muziki, alishirikiana na wasanii wenye majina makubwa kama Jay Z, Erykah Badu, Q-Tip na wasanii wengine akiacha alama isiyofutika katika ulimwengu wa muziki wa R$B.