
Nadia Nakai, rapa wa Afrika Kusini amefunguka kuhusu maisha yake ya mapenzi.
Nadia amesema kuwa kwa sasa asingetaka tena kuingia kwenye uhusiano na rapa mwingine au mtu yeyote katika tasnia ya muzika na kwamba anataka kuwa na uhusiano wenye faragha.
Kauli yake inafafanua wazi kuwa Nadia anathamini sana faragha yake na anataka kujenga uhusiano wa kweli bila kuingiliwa na tasnia ya burudani.
Nadia amewahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na marehemu rapa AKA kutoka Afrika Kusini.