
Msanii maarufu wa Bongo Fleva, @marioo_tz, amepata nafasi ya kuzingatiwa na Recording Academy baada ya wimbo wake “Nairobi”, alioufanya kwa kushirikiana na @bienaimesol kuingizwa kwenye orodha ya nyimbo zinazozingatiwa (For Your Consideration) katika tuzo za Grammy.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Marioo alionyesha furaha yake akisema:“Shukrani maalum kwa @recordingacademy kwa heshima na utambuzi wa ‘NAIROBI’ Ndugu yangu @bienaimesol kazi tumeifanya, Asante kwa kila mmoja aliyesaidia @badnationtz.
Wimbo huo, uliopata mapokezi makubwa ndani na nje ya Afrika Mashariki, unaendelea kuthibitisha ubora wa Marioo na mchango wake katika kukuza muziki wa Bongo Fleva nje ya Tanzania.
Hii ni hatua nyingine kubwa kwa muziki wa Tanzania, ikionesha jinsi wasanii wake wanavyofanikiwa kuvuka mipaka ya Afrika kupitia ubunifu na kazi zilizo bora.