Msanii wa Bongo Fleva na mmiliki wa lebo ya African Princess Nandy ameonyesha moyo wa Asante Baba kwa kijana Marik aliyekutana nae mtaani akiuza mayai na kuahidi kumsaidia mtaji na chumba cha kuishi ili aanze maisha.
Ahadi hiyo ya Nandy imetimia baada ya kushare video kwenye ukurasa wake wa Instagram akionyesha tayari amempangishia chumba kijana huyo na kumpatia mtaji wa kuuza mayai kama alivyomuahidi hapo awali.
Nandy ameendelea kuishi sambamba na wimbo wake mpya uitwao “Asante Baba” unaosisitiza kutoa shukrani kwa Mungu kwa chochote hata kama ni kidogo.
Akizungumza na Marik Nandy amemsisitiza awe makini na kuwa kijana mwenye heshima na ajikite kupambania maisha.
