Rapa NBA YoungBoy, anayejulikana pia kama YoungBoy Never Broke Again, amefanikiwa kupata mtoto wa kike siku ya jana na kufanya kufikia idadi ya watoto 13.
Mtoto wa kike aliyezaliwa ni mtoto wa tatu wa YoungBoy na mkewe, Jazlyn Mychelle, rapper huyu alitoa habari hizo za furaha na mashabiki wake kupitia chapisho la mtandao wa kijamii.
YoungBoy alisikika akisherehekea kuzaliwa kwa bintiye, huku mkewe akieleza kufarijika baada ya kujifungua.
Wanandoa hawa wamepokea ujumbe wa pongezi kutoka kwa wapendwa wao na mashabiki wengi kote duniani.
YoungBoy hapoi kabisa, sasa sijui nambari zake zitaenda mpaka ngapi, Rapa huyu bado anaonyesha bado mwendo anauweza na atazidi kupiga hatua hadi pale atakapochoka.
