Nicki Minaj ameligusa jukwaa la Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York baada ya kutoa hotuba yenye uzito kuhusu uhuru wa kuabudu na ukatili unaoripotiwa kutokea dhidi ya Wakristo nchini Nigeria.
Akizungumza mbele ya mabalozi, viongozi wa dini na wawakilishi wa Marekani katika kikao hicho maalum, Nicki Minaj alisisitiza kuwa suala la kulinda waumini nchini Nigeria halipaswi kuonekana kama upande wa kisiasa bali juhudi za kulinda utu wa binadamu.
Katika hotuba hiyo, aligusia umuhimu wa dunia kusimama pamoja kukemea mashambulizi, utekaji na mauaji yanayoripotiwa, akisisitiza kuwa vurugu hizo ni tatizo la kibinadamu na si la kikabila wala kisiasa.
Nicki pia aliwahimiza viongozi wa kimataifa kuhakikisha uhuru wa dini unalindwa kwa kila mtu bila kujali anapotoka au anachoamini, akisema:“Uhuru wa kuabudu ni haki ya kila mmoja wetu kutamka imani yako bila woga.”
Hotuba ya Nicki Minaj imezua gumzo kimataifa kutokana na uzito wa ujumbe wake na nafasi yake kama msanii mkubwa duniani kuzungumzia masuala ya Afrika, jambo ambalo limewafanya wengi kusifu ujasiri wake