
Rapa Nicki Minaj amemjibu Cardi B, ambaye amemuita “Barney B baada ya kumshutumu kwa kuishi maisha ya uongo, matatizo ya ndoa, na kumkejeli kwa mada nyeti kama uzazi Kupitia tweets kali.
Kwenye tweets zake, Nicki amendika:“Je mimi ndiye Barney B na FLOP? Je mimi ndiye ninayesema uongo kuhusu matatizo ya uzazi wakati Malkia hajawahi kumuona wala kuzungumza na daktari wa uzazi maishani mwake? Je mimi ndiye nitakayepelekwa mahakamani Malkia atakapoonyesha rekodi zake za kitabibu? Desiree nina rekodi zako za kitabibu pia Wanasheria wamesema tutamfanya Barney b awe hana makazi ndani ya miezi 36. Tumshukuru Mungu. Kwa sasa tunakula keki.”
Akiongeza, Nicki alimshambulia Cardi kwa madai ya ndoa yenye misukosuko:
Hata hivyo, Nicki pia alionyesha msimamo wa huruma kwa wanawake wanaopitia changamoto za uzazi, akisema:“Pia niseme hivi, ingawa sijawahi kupata matatizo ya uzazi, sio jambo la kutumiwa kama kejeli, Mpaka umjue mwanamke ambaye anaishi na maumivu hayo, akijilaumu mwenyewe tunaweza tu kuwazia na kuwaombea, kuwapenda, kuwainua.
Mvutano kati ya Nicki Minaj na Cardi B ni wa muda mrefu, na mara kwa mara hujitokeza hadharani kupitia nyimbo na mitandao ya kijamii.
Tukio hili jipya limeendeleza mjadala mkali kati ya mashabiki wao, likionyesha kuwa “vita ya malkia wa rap” bado ipo hai na haina dalili za kuisha.