
Muimbaji nyota wa R&B kutoka Marekani, Mario, ameomba radhi hadharani baada ya video kusambaa ikimuonyesha akimfukuza cameraman jukwaani wakati wa show yake huko Fresno Fair, California.
Tukio hilo limezua mjadala mitandaoni huku mashabiki wakimkosoa kwa ukosefu wa subira na ustahimilivu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mario ameeleza kuwa hakujulishwa kuhusu uwepo wa cameraman huyo kabla ya kupanda jukwaani, akisema aliingia dakika kumi tu kabla ya kuanza kutumbuiza.
Aidha amedai cameraman huyo alikuwa amesogea sana mbele ya jukwaa, jambo lililomchanganya na karibu ajikwae wakati akitumbuiza.
Amekiri kuwa alikasirika na kutoa maneno makali, lakini akakubali kosa hilo kwa unyenyekevu:
Mario alimuomba radhi cameraman huyo, akisisitiza kuwa haikuwa chuki binafsi
Amemalizia kwa kuwashukuru mashabiki waliomuunga mkono licha ya tukio hilo na kuahidi kuendelea kuwa msanii mwenye nidhamu.
Mashabiki wameupokea msamaha huo wa Mario kwa mitazamo tofauti ambapo licha ya wengi kumsamehe, wapo wanaodai kuwa haujawa wa dhati kwa cameraman huyo.