
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amefariki dunia leo Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025, akiwa na umri wa miaka 88.
Taarifa rasmi kutoka Vatican News imethibitisha kuwa Papa Francis alifariki akiwa katika makazi yake ya Casa Santa Marta, ndani ya jiji takatifu la Vatican.
Papa Francis, ambaye alizalivwa mwaka 1936, alikuwa kiongozi wa 266 wa Kanisa Katoliki tangu alipochaguliwa rasmi mnamo Machi 13, 2013, kufuatia kujiuzulu kwa mtangulizi wake, Papa Benedict XVI.
Uongozi wake ulijulikana kwa kuhimiza huruma, haki za wahamiaji, mapambano dhidi ya ufisadi, na kujikita katika kulisemea kanisa lisiwe mbali na watu wa kawaida.
Tangu kuanza kwa utume wake kama Papa, Francis alijitokeza kama kiongozi wa mabadiliko na mshauri wa amani duniani, akisisitiza maisha ya unyenyekevu na utumishi kwa maskini.
Mchakato wa maandalizi ya mazishi unatarajiwa kutangazwa hivi karibuni na viongozi wa Vatican.