Mpenzi wa msanii Phina, Eni, ameandika ujumbe wa hisia nzito uliowagusa mashabiki wengi, akieleza hofu, matumaini na hatua mpya anayoingia kwenye maisha yake ya ubunifu na muziki.
Kwenye ujumbe huo, Eni amekiri kuwa ana hofu, lakini sio hofu ya kuonewa huruma, bali hofu inayokuja pale mtu anapokaribia kuanza jambo jipya. Ameeleza kuwa muziki ni aina mpya ya sanaa kwake, jambo linalomfanya ajisikie tofauti ukilinganisha na kazi alizowahi kufanya hapo mwanzo.
Eni pia amefafanua sababu ya kupungua kwa uwepo wake mitandaoni, akisema amekuwa akifanya kazi kubwa zaidi ya kawaida, hasa nyuma ya pazia la utayarishaji wa muziki. Amebainisha kuwa kutengeneza muziki sio kuandika au kuimba nyimbo pekee, bali ni mchakato mrefu na wenye kazi nyingi.
Cha kuvutia zaidi, Eni amethibitisha rasmi kuwa yeye na Phina wameunda bendi ndogo iitwayo @eniandphina, na tayari wameandaa nyimbo nyingi pamoja. Kwa mujibu wa Eni, hatua ya kuandika ujumbe huo ilimfanya ahisi kuwa safari ya muziki wao sasa imeanza rasmi.
Akiwaomba mashabiki wake msaada, Eni amewahimiza kusikiliza na kuunga mkono muziki wao pindi utakapotoka, akisema kuwa licha ya hofu zake, anaamini kazi waliyoifanya ni nzuri sana.
Ujumbe wake aliuhitimisha kwa shukrani kwa mashabiki wake, akisisitiza kuwa hawawaoni kama mashabiki tu bali kama marafiki wa kweli waliompa nguvu kee kila hatua ya safari yake.