
Msanii wa Bongo Fleva Phina ametangazwa rasmi kuwa msanii mpya wa Apple Music Up Next East Africa, programu inayotambua na kukuza vipaji vipya barani Afrika.
Kupitia tangazo hilo, @phina__tz ameonyesha furaha yake kubwa akisema anaheshimu kuwa miongoni mwa wasanii wapya bora wanaowakilisha muziki wa kizazi kipya.
Mashabiki wanaweza kusikiliza nyimbo zake kupitia “UpNext playlist ya Apple Music”, ikiwemo “Sisi Ni Wale” wimbo uliotikisa TikTok kwa zaidi ya video milioni 1.6.
Hii ni hatua muhimu kwa Phina, ikithibitisha nafasi yake kama mmoja wa wasanii wanaoendelea kuipeleka Bongo Fleva kimataifa.