
Jeshi la Polisi wilayani Kasulu mkoani Kigoma limepiga marufuku watoto kufanya biashara kwenye masoko ya usiku ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyoweza katisha ndoto zao.
Marufuku hiyo imetolewa na Mkaguzi msaidizi wa jeshi la Polisi wilaya ya Kasulu Mbaraka Luwongo jana katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika na kuwataka wazazi na walezi kutokuwa chanzo cha watoto wao kutembea usiku.
Luwongo amesema wazazi na walezi wanapaswa kuwa walinzi kwa watoto kutokana na uwepo wa matukio mbalimbali ya vitendo vya ubakaji na ulawiti na kuwajengea mazingira ya kujisomea wakaeti wote
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kasulu Sabinus Chaula amewataka watoto kutoa taarifa kwa waalimu,wazazina ndugu wa karibu wanapofanyiwa vitendo vya ukatili ili hatua za kisheria zichukuliwe kudhibiti matukio hayo.