
Prisca wa BSS ametoa shukrani za dhati kwa wazee na wananchi wote wa Tanzania waliokuwa sehemu ya safari yake ya Bongo Star Search, Season 15, 2025.
Prisca alifanikiwa kufikia nafasi ya nne miongoni mwa washiriki kutoka nchi za Afrika Mashariki, jambo ambalo linatokana na upendo na kuungwa mkono na mashabiki wake.
Prisca amesema“Nia yangu ya sadaka hii kwa wazee ni kuwashukuru wote waliokuwa wakiniunga mkono wakati wa mashindano ya Bongo Star Search na safari ya shukrani hii haitaishia hapa, nitakuwa nikiendelea kugusa makundi mbalimbali yenye mahitaji maalumu,”
Aidha, Prisca ametumia fursa hii kuomba msaada kutoka kwa wadau pale atakapokuwa anaachia kazi zake mpya, akiahidi kuwa kazi zake zitaleta burudani na kwa mashabiki wa muziki wake