
Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Raila Odinga amefariki dunia leo kutokana na shambulio la moyo akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali moja nchini India.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Nation cha nchini Kenya, taarifa za kifo cha Odinga ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), zimethibitishwa na mmoja wa wasaidizi wa ofisi yake.
Odinga alihudumu kama Waziri Mkuu wa Kenya katika serikali ya mseto ya mwaka 2008 hadi 2013.
Kabla ya kuwa Waziri Mkuu alikuwa Mbunge wa Lang’ata kuanzia 1992 hadi 2007, kisha akahudumu kwenye Baraza la Mawaziri la Kenya kama Waziri wa Nishati kuanzia 2001 hadi 2002, na baadaye kama Waziri wa Barabara, kazi ya umma na makazi kuanzia 2003 hadi 2005, na kisha akateuliwa kuwa Mwakilishi wa juu wa maendeleo ya miundombinu katika Umoja wa Afrika mwaka wa 2018.
Raila Odinga alizaliwa January 7, 1945 amewania urais mara tano – mwaka wa 1997, 2007, 2013, 2017 na 2022 – akibaki mmoja wa viongozi wa upinzani wenye ushawishi mkubwa na mtetezi wa mageuzi nchini Kenya.