Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaonya wafanyabiashara dhidi ya kutumia mwanya wa kupanda kwa bei ya mafuta kupandisha bei za bidhaa kupita kiasi, akisisitiza umuhimu wa kuzingatia uhalisia wa gharama.
Akizungumza leo Jumatano, Aprili 8, 2026, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati wa kuwaapisha viongozi wapya aliowateua.
Amesema kuwa ongezeko la bei ya mafuta linatokana na hali ya kimataifa na si maamuzi ya Serikali ya Tanzania, akibainisha kuwa bado bei ya mafuta nchini iko chini ikilinganishwa na mataifa mengine.
katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza hatua ya kupunguza matumizi ya mafuta serikalini kwa kuanza na ofisi yake, akisema kuanzia sasa viongozi wakubwa watapanda pamoja katika basi moja badala ya kila mmoja kutumia gari lake.
Amesema msafara wake utakuwa na ulinzi wa kawaida, ukiwemo msafara wa polisi (escort) pamoja na gari ya akiba nyuma, lakini idadi ya magari ya viongozi itapunguzwa kwa kiasi kikubwa.
