
Na Michael Mpunije- Kasulu, Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka watumishi wa Umma wilayani Kasulu kubuni vyanzo mbalimbali vya utalii ili kuongeza pato la Taifa kupitia Sekta hiyo.
Ametoa Wito huo leo wakati akizungumza na watumishi wa umma viongozi wa dini pamoja na viongozi wa vyama vya siasa katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu.
Aidha Balozi Sirro amezitaka halmashauri za wilaya ya Kasulu kufanya kazi kwa ushirikiano kubuni vyanzo vya utalii ambavyo vitasaidia kuongeza fedha za kigeni pamoja na kukuza uchumi wa halmashauri.
Balozi Simon Sirro anaendelea na Ziara yake ya kikazi katika halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma ambapo kwa wilaya ya Kasulu ametoa maelekezo mbalimbali kwa watumishi wa umma kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi.