
Mwanamuziki nyota wa muziki wa Pop duniani, Rihanna na mpenzi wake A$AP Rocky, wamejaaliwa mtoto wa tatu, ambaye ni binti, huko nchini Marekani, mtoto huyo amepewa jina la kisanii la baba yake.
Ujio wake umetangazwa kupitia ukurasa wa Instagram wa Rihanna, uliokuwa na picha za kifamilia pamoja na glovu ndogo za ndondi za rangi ya waridi.
Kwa wawili hao, hii ni familia ya tatu baada ya watoto wawili wa kiume, Riot na RZA, Rihanna alitangaza ujauzito wake hivi karibuni wakati wa hafla ya Met Gala mwaka huu.
Habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo zimepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki duniani kote, ambapo chapisho la Rihanna mtandaoni limevutia zaidi ya likes milioni tano ndani ya saa mbili.
Mbali na muziki, Rihanna mwenye umri wa miaka 37 amejipatia mafanikio makubwa kwenye biashara kupitia chapa yake ya urembo, Fenty Beauty, na kampuni ya mavazi ya ndani.
Jarida la Forbes linakadiria thamani yake kuwa zaidi ya dola bilioni moja, jambo linalomfanya kubaki katika orodha ya wanawake maarufu na wenye ushawishi mkubwa duniani.