Msanii mkongwe wa muziki wa Injili, Rose Muhando, ameibuka na kauli nzito akiwapinga vikali watu wanaohusisha mavazi au rangi nyeusi na nguvu za giza, laana au uchawi.
Akizungumza kwa msisitizo, Rose Muhando amesema watu waache kuhukumu rangi nyeusi, akibainisha kuwa si ishara ya laana wala uchawi wa aina yoyote. Kwa mujibu wake, kauli hizo hutolewa na watu wanaoongea bila kumjua Mungu.
Rose Muhando pia amekemea vikali imani potofu zinazowafanya watu kufikia hatua ya kujichubua au kubadili rangi ya ngozi, akisisitiza kuwa nyeusi ni rangi kama nyingine yoyote na haimaanishi chochote katika ulimwengu wa Roho.