
Mtayarishaji muziki, ajulikanaye kwa jina la Bakteria, amepata changamoto kubwa kiafya baada ya kushambuliwa na vibaka karibu na studio yake katika mji wa Tanga, jambo ambalo limepelekea kupooza na kushindwa kutembea kwa takribani miaka miwili.
S2Kizzy, ambaye ni mtayarishaji anayepewa umakini sana, amemtembelea Bakteria na kumpelekea msaada wa kiroho na kimwili ili kumtia nguvu na kumpa matumaini ya kuendelea na ndoto zake.
S2Kizzy amesema, kuwa Bakteria ndiye alikuwa msaada mkubwa kwa familia yake kupitia kazi za production, lakini sasa hali imemlazimisha kusimama, Ni muhimu tuungane pamoja kusaidia ndugu zetu wanaopitia changamoto.
Bakteria anaishi na mama yake mzazi ambaye pia ana changamoto za kiafya, jambo ambalo limeongeza mzigo wa familia yao. @S2Kizzy ametoa wito kwa mashabiki na jamii kusaidia
Hali ya Bakteria inakumbusha jamii kuwa kusaidiana ni muhimu, na kwamba msaada wa pamoja unaweza kumfanya mtu kurejea kwenye maisha yake ya kawaida na ndoto zake.