Mvutano mkubwa umeibuka ndani ya soka la Afrika nahodha wa timu yua taifa ya Senegal, Sadio ManΓ©, ameripotiwa kukataa ombi la CAF la kumtaka arejeshe tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Mashindano (MVP) ya AFCON 2025.
Hii inakuja baada ya CAF kuipokonya Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuipa Morocco, kufuatia tukio la wachezaji wa Senegal kugoma kurudi uwanjani kwa dakika 17 wakati wa fainali ya Januari 18, 2026.
ManΓ© amesema : “Nalinda heshima ya nchi yangu. Tuzo hii nimeipata uwanjani kwa jasho na damu, siyo kwenye chumba cha mikutano (boardroom).”

Ulinzi Mkali: Inasemekana tuzo hiyo na Kombe la AFCON 2025 vimepelekwa kuhifadhiwa kwenye kambi ya kijeshi nchini Senegal kuzuia visichukuliwe.
Msimamo wa Hakimi: Licha ya Morocco kupewa ubingwa, beki Achraf Hakimi ameripotiwa kuukataa akisema Senegal walishinda kihalali uwanjani.
CAS: Shirikisho la Senegal (FSF) limefungua kesi rasmi katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kupinga uamuzi huo.
CAF sasa inapanga kumpa tuzo hiyo ya MVP mchezaji wa Morocco, Brahim DΓaz.
