
Wimbo mpya wa Diamond Platnumz uitwao Sasampa, aliomshirikisha Focalistic, Silas Afrika na Uncool MC, umeendelea kufanya vizuri mitandaoni, ukishika namba moja kwenye Instagram trending audios.
Inaonekana kuwa original audio ya Sasampa kwenye Instagram inaonyesha jina la iamlavalava kama msanii mkuu aliyeachia wimbo huo badala ya Diamond mwenyewe.
Hii inaweza kuchanganya watu wakidhani Lava Lava amehusika kwenye uimbaji au utayarishaji wa wimbo huo, ingawa kila kitu rasmi kinamtaja Diamond Platnumz kama msanii mkuu, akishirikiana na Focalistic, Silas Afrika na Uncool MC pekee.
Hii inaweza kuwa hitilafu ya wasambazaji wa muziki mtandaoni, Mara nyingi, majukwaa kama Instagram hutegemea taarifa kutoka kwenye metadata za nyimbo zinazopandishwa kupitia kampuni za usambazaji.
Inaonekana katika mchakato huo, jina la Lava Lava lilijikuta likiwa kwenye sehemu ya msanii wakati wimbo ulipopandishwa, na hivyo Instagram ikaonyesha akaunti yake kama chanzo cha original audio.
Pamoja na mkanganyiko huo wa majina, Sasampa imeendelea kutamba, ikitumika kwenye maelfu ya reels ndani ya siku chache na kuongoza kwenye Instagram trending audios.Diamond mwenyewe aliwashukuru mashabiki kwa mafanikio hayo