
Huduma ya kivuko cha Mayenzi– Kanyinya inatarajiwa kuanza kutolewa wakati wowote kuanzia sasa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za muda mrefu za kuimarisha miundombinu ya usafiri katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Huduma hii inatarajiwa kusaidia wananchi na biashara zao kuvuka kwa urahisi kati ya Mayenzi na Kanyinya, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo walilazimika kutumia mitumbwi.
Mbunge wa Jimbo la Ngara, Bw. Ndaisaba Ruhoro, amewashukuru viongozi wote waliosimamia utekelezaji wa mradi huu, akiwemo Mkuu wa Wilaya Kanali Mathias Kahabi.
Aidha Mbunge Ruhoro amesema hatua hii ni utekelezaji wa ahadi ya muda mrefu kwa wananchi wa maeneo hayo.
Ikumbukwe kivuko hicho kinajengwa kupitia fedha zilizotolewa na serikali kuu.