Waziri wa Madini Bw Anthony Mavunde ameielekeza Tume ya Madini nchi kufuta leseni 73 za uchimbaji wa kati na utafiti wa madini ambazo hazijaendelezwa.
Waziri Mavunde ametoa maelekezo hayo leo wakati akiongea na vyombo ya habari katika ukumbi wa Ofisi za Tume ya Madini mjini Dodoma.
Amesema kuwa, ufutaji wa leseni hizo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuiwezesha Wizara ya Madini kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuhakikisha malengo yanafikiwa na lasilimali madini kuwanufaisha Watanzania.
Waziri Mavunde ameeleza kuwa, Leseni zilizofutwa ni pamoja na leseni za utafutaji wa madini 44 na leseni 29 za uchimbaji wa kati kutokana na kushindwa kurekebisha makosa yao.
Kuhusu matumizi ya maeneo yote yaliyofutwa, Mavunde amesema kuwa, maeneo hayo yatapangwa kwa ajili ya mradi wa vijana katika programu ya Mining Better Tomorrow (MBT) ili waweze kunufaika na rasilimali madini.