
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, imetupilia mbali Shauri la Kikatiba Namba 24027 la mwaka 2025 lililofunguliwa na mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, pamoja na chama hicho, wakipinga kuondolewa kwenye orodha ya wagombea wa urais.
Hukumu hiyo imetolewa leo, baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote mbili.
Katika maamuzi yake, Mahakama imeeleza kuwa haina mamlaka ya kuhoji au kuchunguza jambo lolote linalotekelezwa na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) katika utaratibu wake wa kikatiba na kisheria, bila kuingiliwa na chombo chochote.
Akizungumza mara baada ya hukumu hiyo Kaimu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Mbarala Maharagande, amesema chama hicho kitatoa msimamo wake rasmi baada ya kupitia hukumu hiyo kwa kina.
Shauri hilo lilisikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Frederick Mayanda, huku upande wa waleta maombi ukiongozwa na Wakili John Seka na timu yake ya mawakili.
Wadaiwa katika shauri hilo walikuwa ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali