Shafiru Yusuph- KAGERA
Shirika la kwa Wazee limetoa jumla ya baiskeli 400 kwenye shule 13 za Sekondari katika wilaya tano za Mkoa wa Kagera kwa wanafunzi wanaotembea umbali wa zaidi ya kilomita tano.
Akibabidhi baiskeli hizo Afisa Miradi wa Shirika la kwa Wazee Bw. Edmund Revelian amesema kuwa lengo la kugawa baiskeli hizo bure ni baada ya wanafunzi kushindwa kuhudhuria vipindi vya darasani kwa wakati.
Amesema kuwa wilaya ambazo zimepokea msaada huo ni wilaya ya Muleba baiskeli 50, Bukoba baiskeli 100, Misenyi baiskeli 100, Biharamulo baiskeli 50 na Wilaya ya Karagwe 100.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibanga Mwl. Rwakailima Cladius ambaye amepokea baiskeli 25 amesema kuwa baiskeli hizo zitaongeza chachu ya ufaulu kwa wanafunzi kwani waliowengi wanaishi mazingira ambayo sio rafiki na yapo mbali na shule.
Baadhi ya wanafunzi waliopatiwa baiskeli wameshukuru Shirika hilo kwani awali walikuwa wakiamka saa kumi na moja alfajiri kwenda shule na kufika saa moja na nusu hadi saa mbili na kusababisha kukosa baadhi ya vipindi vya darasani.
