
Zaidi ya wanafunzi 800 wa shule ya msingi Ruziba iliyoko wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera wameondoka na changamoto ya kupanga foleni wakati wa kwenda kujisaidia katika choo kimoja na wengine kulazimika kujisaidia vichakani baada ya shirika la Sanitation and woter Action SAWA kuwajengea matundu 11 ya vyoo vipya vya kisasa kwa ufadhili wa shirika la UNICEF na serikali.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ruziba Bw Skalion George amesema hayo wakati anazungumza na Radio Kwizera juu ya changamoto zilizokuwa zinakabili shule hiyo na kupelekea wanafunzi kushindwa kujifunza kwa ubora kutokana na changamoto hiyo.
Amesema upungufu wa matundu ya vyoo katika shule hiyo yenye wanafunzi 847 wanafunzi wa kiume 403 na wasichana 444 ambapo kabla ya ujenzi wa matundu 11 ,na matundu 10 kukarabatiwa uwiani wa wanafunzi 80 walikuwa wakitumia dundu moja la choo jambo ambalo lilikuwa linasababisha msongamano.
Katibu tawala wa wilaya ya Biharamulo Bw Kasimu Kirondomara ameitaka halmashauri kwa kushirikiana na jamii kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo kwenye shule zilizo na upungufu wa vyoo kabla ya madhara kutokea katika shule hizo.