
Baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutoa orodha ya vilabu bora Afrika kwa viwango vya CAF Klabu ya Simba SC ya Tanzania imeendelea kusalia kwenye 10 bora ikishikilia nafasi ya 5 nyuma ya vinara Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Esperance Tunis na RS Berkane.
Katika orodha hiyo Tanzania imeingiza timu 3 kwenye orodha ya vilabu 75 bora barani humo ikiwemo Simba Sc (alama 48) nafasi ya 5, Yanga (alama 34) nafasi ya 12 na Namungo FC (alama 0.5) nafasi ya 75 ikifungana kwa alama na vilabu vingine vitano.
Orodha hiyo inakuja kuelekea droo ya hatua ya michuano ya CAFCL na CAFCC itakayofanyika Agosti 9, 2025.
Hakuna timu yoyote kutoka Kenya iliyoingia kwenye vilabu 100 bora barani Afrika huku Simba SC ikishikilia usukani kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA, Yanga Sc nafasi ya pili, Vipers ya Uganda nafasi ya tatu na Namungo FC nafasi ya nne na ndio vilabu vinne pekee vilivyopo kwenye top 100 ya CAF kutoka CECAFA.
VILABU 10 BORA AFRIKA
- Al Ahly (78)
- Sundowns (62)
- Esperance (57)
- Berkane (52)
- Simba Sc (48)
- Pyramids (47)
- Zamalek (42)
- Wydad AC (39)
- USM Alger (37)
- CR Belouizdad (36)