
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Shinyanga imeokoa shilingi milioni 92.16 kati ya Shilingi milioni 151.53 zilizokuwa zimeibiwa na viongozi wa chama cha msingi cha Ibambala AMCOS kilichopo halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.
Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Bw. Donasian Kessy wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo katika kipindi cha Robo ya tatu ya kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.
Aidha Bw. Kessy amesema kuwa wamefikia mafanikio hayo kutokana na ushirikiano walioupata kutoka kwa wananushirika wa chama hicho.
Katika hatua nyingine Bw. Kesy amesema kuwa kuelekea uchaguzi mkuu wamejipanga kudhibiti vitendo vya Rushwa ambavyo vinafanywa na baadhi ya watia nia watakao bainika kujihusisha na
vitendo hivyo.