Waziri wa Nishati wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameshiriki mazungumzo ya ngazi ya juu mjini Paris, Ufaransa, yaliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA). Mazungumzo yamelenga mikakati ya kupanua upatikanaji wa nishati kwa wote na kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kutoa nishati endelevu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii

Picha ya pamoja na viongozi waliohudhuria mkutano huo Paris nchini Ufaransa msitari wa mwisho katika picha aliyevalia shati nyeupe ni Waziri wa Nishati wa Tanzania, Deogratius Ndejembi .
