
Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) kimesema kuna dalili na viashiria vya hali ya mgawanyiko wa kisiasa, kidini na kikabila yanayopapaswa kukemewa vikali kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.
Hayo yamesemwa na Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi jana Jumanne, Agosti 26, 2025 alipozungumzia juhudi ambazo TLS imezichukua kuhakikisha kunakuwa na maridhiano na mshikamano wa kitaifa kuelekea uchaguzi huo.
Amebainisha kuwa dalili na viasharia hivyo vimeanza tangu changuzi za mwaka 2019, 2020 hadi 2024.
Akitolea mfano wa kaulimbiu za vyama kuelekea uchaguzi huo, amesema siyo zilizozoeleka, akitolewa mfano, kuwa wapo wanaosema ‘Oktoba Tunatiki’, ‘No Reforms no Election’, na ‘Piga kura linda kura’ amedai kauli hizi zinaonyesha changamoto katika mfumo wa kiuchaguzi.