
Mkuu wa wilaya ya Geita mkoani humo Hashim Komba amevitaka vikundi vya wajasiriamali ambavyo vimepatiwa mikopo, kuhakikisha mikopo hiyo inayotumika katika kutekeleza malengo ya kuinua uchumi
Komba amesema hayo wakati akikabidhi hundi ya mkopo kwa vikundi mia moja kumi na moja vya wanawake, vijana na wenye ulemavu, hafla ambayo imefanyika makao makuu ya halamashauri hiyo kwenye kata ya Nzera
Amesema serikali inatoa fedha hizo ili ziwe sehemu ya kukuza uchumi kwa wajasiriamali, hivyo ni vema fedha hizo ziongeze uzalishaji na kurejeshwa kwa wakati ili vikundi vingine viweze kukopeshwa
Halmashauri hiyo ya wilaya ya Geita imetoa hundi ya mkopo wa shilingi bilioni 1 na milioni 156 kwa vikundi vya wajasiriamali ikiwa ni mikopo ya aslimia 10 ya mapato ya ndani ya halamshauri.