Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, amekutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, kufuatia Misa ya hija iliyofanyika Vatican.
Mkutano huo mfupi ulifanyika mara baada ya ibada iliyohudhuriwa na mahujaji na viongozi kutoka sehemu mbalimbali duniani, ukionesha ushiriki wa Tanzania katika majukwaa ya kimataifa ya kidini na kidiplomasia.

Vatican imeendelea kuwa kitovu muhimu cha imani ya Kikatoliki duniani, ikivutia waumini na viongozi wengi kila mwaka kushiriki katika matukio makubwa ya kidini.
Ushiriki wa Dk. Nchimbi ni juhudi za Tanzania kuendelea kuimarisha uhusiano wake na Jumuiya ya Kikatoliki duniani pamoja na kukuza mazungumzo ya kidini na ushirikiano wa kimataifa.
