
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi linafahamu umuhimu wa kuwepo mazingira ya amani, utulivu, haki, na kuheshimu misingi ya demokrasia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Amesema hayo wakati akizungumza leo Agosti 20,2025, katika mdahalo uliohusu amani, haki, na demokrasia uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira ya usalama na litasimamia masuala ya haki, amani, na utulivu, huku likipambana na vitendo vya uhalifu vinavyoweza kusababisha vurugu wakati wa uchaguzi.
Pia, Kamanda Muliro amewakumbusha wananchi kuhusu wajibu wao wa kutii sheria na kulinda amani ya Taifa.