
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Geita imesema kuwa imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 62.9 kiasi ambacho ni zaidi ya malengo
Meneja wa TRA mkoa wa Geita Elirehema Kimambo ameeleza mafanikio hayo katika uzinduzi wa dawati maalumu la uwezeshaji wafanyabiashara linalolenga kuwawezesha wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari
Kimambo amesema malengo yalikuwa ni kukusanya bilioni 61.7 lakini mamlaka imevuka malengo na kukusanya bilioni 69.2 sawa na asilimia 103
Kaimu mkuu wa mkoa wa Geita ambaye ni katibu tawala wa mkoa huo bw. Mohamed Gombati amewapongeza watumishi wa TRA kwa kufanya kazi hiyo kwa ufanisi pasipo na malalamiko kwa wafanyabiashara