Marco Pastory & Amina Semagogwa– Ngara, KAGERA
Vijana Wakatoliki Wafanyakazi VIWAWA Parokia ya Ngara mjini wameshiriki matendo ya huruma kwa kumtembelea kijana mwenzao ambaye ni mgonjwa kwa zaidi ya miaka 10.
Wakiwa na vitu mbalimbali vya mahitaji ya binadamu VIWAWA hao wamemtembelea kijana Dickson Kizito ambaye alipata changamoto ya kiafya na kumfanya asiweze kunyanyuka wala kutembea toka akiwa na umri wa miaka 7.

Mlezi wa VIWAWA Padre Vedasto Ademba amewataka vijana kuendelea kufanya matendo ya huruma kwa wenye uhitaji na isiishie kipindi cha Kwaresma pekee huku akiwasihi kuendelea kumwombea kijana Dickson.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa VIWAWA Jerald Msoke amewashukuru vijana kwa kujitokeza na kumfariji kijana mwenzao, huku familia ya kijana Dickson ikishukuru kwa majitoleo waliyofanya.
