Enock Yoronimo- BUKOBA, KAGERA
Kupatikana kwa mashine ya ‘photocopy’ katika Shule ya Msingi Bunena kumeelezwa kuwa na athari chanya kwa walimu na wanafunzi ikiwemo kuongeza ujifunzaji kwa wanafunzi.
Hatua hiyo ni kutokana na juhudi za pamoja kati ya Mbunge wa Bukoba Mjini, Johnstone Mutasingwa, Diwani wa kata ya Bakoba Shaban Rashid na wananchi baada ya kuchangia mashine ya ‘photocopy’.

Mkuu wa shule hiyo, Devotha Mugisha, amesema sasa wanafunzi watajifunza kwa urahisi zaidi kutokana na upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia.
Baadhi ya walimu katika shule hiyo wamesema kuwa wataondokana na changamoto ya gharama na usumbufu wa kutafuta huduma za uchapishaji nje ya shule.
