Wabunge nchini Burundi wamesema kuna hatari ya kufirisika kwa Taasisi ya Uzalishaji wa zao la Michikichi OHP, kutokana na changamoto kubwa ya kifedha ndani ya taasisi hiyo.
Wabunge hao wameeleza hayo kupitia ripoti iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Mahakama ya Ukaguzi inaonesha fedha zilizotolewa na OHP kati ya mwaka 2012 hadi 2018 bado hazijarejeshwa kama ilivyotarajiwa.
Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2003 hadi 2014 OHP iliuza miche ya chikichi kwa faranga za Burundi bilioni 93 na ni bilioni tano pekee zilizokusanywa hadi sasa.
Akijibu maswali bungeni Ijumaa ya wiki iliyopita Waziri wa Kilimo nchini Burundi Calinia Mbarushimana amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na ameahidi wabunge kuwa serikali tayari imeanza kuchukua hatua.
Mbunge Ledamtel Gahitira amesema mapato yaliyokusanywa na OHP mwaka 2024–2025 ni madogo ukilinganisha na makadirio yaliyotalajiwa na uongozi wa taasisi hiyo kujitathmini upya na kuchukua hatua stahiki.