
Na, Elias Anthony
BUJUMBURA
Baadhi ya wabunge nchini Burundi wamekosoa mpango wa serikali ya nchi hiyo ya kuwarejesha Sokwe waliopelekwa nchini Kenya wakati wa vita.
Katika kikao cha kawaida cha baraza la Bunge kilichofanyika jijini Bujumbura cha mwishoni mwa wiki wabunge hao wamesema wana mashaka juu ya matumizi ya fedha zilizotengwa kwenye bajeti kuu ya serikali ya mwaka 2024-2025 za kutekeleza mpango wa kurejesha sokwe hao kutoka nchini Kenya.
Wabunge hao akiwemo Agathon Rwasa wamesema hawaelewi sehemu watakapowekwa sokwe hao wakati hata sokwe waliopo nchini humo wanaishi katika mazingira yasio rafiki.
Hata hivyo waziri mkuu wa Burundi Gervais Ndirakobucha amewatoa hofu wabunge hao na kueleza kuwa serikali hiyo inaandaa sehemu ya kuwaweka Sokwe hao kwa manufaa ya taifa.