
Wafugaji mkoani Kigoma wameshauriwa kufanya ufugaji wa kisasa na kufuata taratibu za ufugaji bora ili kuondoa upungufu wa maziwa katika jamii hali inayosababisha baadhi ya wananchi kukosa lishe bora.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kigoma Mganwa Nzota amesema hayo jana alipomuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo Rashid Chuachua katika kilele cha wiki ya unywaji wa maziwa duniani iliyoshirikisha halmashauri nne za mkoa wa Kigoma
Baadhi ya wafugaji na wachakataji wa maziwa wameshauri jamii kutumia maziwa na kuishauri serikali kutengeneza mazingira mazuri ya ufugaji kuendeleza shughuli ya ufugaji mkoani humo.