
JESHI la Polisi mkoani Geita limebaini baadhi ya waganga wa kienyeji na tiba mbadala wanatumia nafasi zao kufanya matukio ya udhalilishaji na ukatili dhidi ya wanawake kwa kisingizio cha matibabu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Safia Jongo amesema hayo katika mkutano wa hadhara Kijiji cha Nyakagomba wilayani Geita.
Amesema uchunguzi umebaini baadhi ya waganga wa tiba asili wanawalazimisha wateja wao wa kike kufanya nao mapenzi na kisha kuwarekodi picha chafu kama kitisho iwapo watatoa siri.
Amesema uchunguzi unaendelea na watakaobainika kuanya hivyo watachukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa mahakamani.
Katika hatua nyingine Kanamnda, amewaonya baadhi ya waganga wa tiba asili wenye tabia ya kupandikiza chuki na kutumia ramli chonganishi kwa wanasiasa.